Bayticol pour-on ni dawa ya kuua kupe kwa ng’ombe inayotumika kwa njia ya kumiminia mgongoni.
Ina Flumethrin 1% m/v katika mchanganyiko tayari kwa matumizi.
• Huzuia kupe, inzi na mbung’o (ndorobo) kwa ng’ombe.
• Rahisi kutumia kwa kumiminia kwenye mstari wa mgongo.
• Hutoa kinga ya muda mrefu.
• Hufanya kupe jike kutozaa.
• Haiondoshwi na mvua.
• Hakuna kipindi cha kusubiri kwa nyama na maziwa.